TEXAS BAR AND NIGHT CLUB NDIO MPANGO MZIMA KWA MAPUMZIKO YA WEEKEND
Leo hii
naungana na watoto hao wa mujini kwa kuwaambia wakazi wa Dar es Salaam na vitongoji
vyake hasa wa Goba kuwa kwa mahitaji ya kupumzika weekend waende Texas Bar and Night Club ambayo imefanyiwa maboresho makubwa iliyopo Goba Center mita 50 kutoka makutano ya barabara ya kutoka Makongo na barabara kuu ya kwenda Mbezi njia ya kwenda Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT) ambapo huduma zote za vyakula zinapatikana.
Meneja wa
Bar hiyo Tito Justine alitaja huduma zinazopatikana katika Bar hiyo kuwa ni
chakula cha aina zote, zikiwepo aina zote za nyama choma inayookwa na wachomaji
wenye uzoefu mkubwa.
Alitaja
mahitaji mengine kuwa ni vinywaji vya kila aina ikiwepo juisi halisi iliyotengenezwa kwa viwango vya
hali ya juu ambayo inapatikana ndani ya dakika mbili baada ya mteja kutoa oda.
Alitaja huduma
zingine kuwa ni ya Cassino, Car Wash, Live Band inayoporomoshwa na Bendi ya
Mwenge Jazz kila Jumamosi huku kukiwa na nafasi kubwa ya kuegesha magari na
kuwa na ulinzi wa kutosha.
Alisema kwa
walaji wa mbuzi katoliki ‘Kitimoto’ pia kinapatikana katika eneo maalumu
lilitengwe katika bar hiyo na kufanya kila mtu kufurahia weekend yake akiwa
katika bar hiyo yenye mandhari na rafiki kwa mapumziko.
Kivutio
kikubwa cha bar hiyo na Night Club ni huduma mbalimbali zinazotolewa na wahudumu warembo na
wa viwango vya juu kama wale wa hoteli
za Nyota Tano huku wakiwa nadhifu na wanaotumia lugha nzuri kwa wateja.
Baadhi ya wateja wameupongeza uongozi wa bar hiyo kwa kuja na maono ya biashara hiyo ambayo imewasogezea huduma za chakula na mahitaji mengine.









Post a Comment