SIMULIZI YA MWANAHARAKATI PATRICK GEORGE MITRI
........................
Naitwa
Patrick George Mitri (55) nimezaliwa Februari, 1970 Kijiji cha Mgila Kata ya
Kwashemshi Wilaya ya Korogwe Vijijini Mkoa wa Tanga.
Mimi ni
Mwanaharakati wa Vita dhidi ya Umasikini.
Kabla ya
kujigundua mimi ni nani nimepitia katika mapito mengi magumu yaliyopelekea
kugundua kilichopo ndani yangu ni nini na hatimaye nikajiita mwanaharakati wa
vita hivyo.
Ilikuwa
mwaka 2003 nilipo jitambua.
Misukumo
iliyokuwa ndani yangu iliongezeka sana baada ya kujitambua nini nani ndani
yangu, misukumo yote ililenga wajibu mkubwa wa kitaifa sikujua la kufanya kwani
yote yaliyondani yangu niliona mzigo mzito ambao sikujua pa kuutua, wala
sikujua nitaanzia wapi na nitamalizia wapi.
“ Dhamira yangu
ilinitisha nakuwaza sina elimu kubwa ya kunipa heshima ya kusikilizwa, sina
fedha za kunipa thamani ya kusikilizwa wala sina umaarufu wowote wa kunipa
kujiamini niliishi kwa mateso na wimbi la mawazo,” alisema Mitri.
Nilikaa
kimya na misukumo ya kitaifa iliyo ndani mwangu tangu mwaka 2003 mpaka 2014
ambapo nilipata msukumo wa kuandika waraka kwa viongozi wa kitaifa wa vyama
vyote vya kisiasa nchini.
Bali nihisi
ugumu sababu tangu nizaliwe sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha
siasa je nikieleza ya siasa nitaeleweka? Kwa maswali niliojiuliza msukumo
ulinilazimisha niandike hatimaye mwaka huo 2014 niliandika waraka huo kwa
viongozi wa kitaifa wa vyama vya kisiasa bali nilishindwa kuwapata viongozi hao
na kuwakabidhi waraka huo kwani niliamini kwa kuwakabidhi mikononi mwao ana kwa
ana ukawa wajibu wangu wa kwanza kuutekeleza.
Simulizi ya kwabza, itaendelea tena kesho kwa maoni piga namba 0717356133.




Post a Comment