Header Ads

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AWATUNUKU VYETI WAHITIMU 6,334 TIA

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula akihutubia katika mahafali ya 23 ya wahitimu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Kampasi za Dar es Salaam, Zanzibar na  Tanga yaliyofanyika Desemba 19, 2025 Makao Makuu ya Taasisi hiyo Kurasini Jijini Dar es Salaam.

..................................

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula amewatunuku vyeti wahitimu 6,334 wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Kampasi za Dar es Salaam, Zanzibar na Tanga katika ngazi mbalimbali kuanzia Cheti cha Awali hadi Shahada ya Uzamili.

 Mhe. Luswetula ambaye alikuwa mgeni rasmi aliwatunuku vyeti hivyo kwenye sherehe ya maafali ya 23 zilizofanyika Desemba 19, 2025 makao makuu ya Taasisi hiyo Kurasini Jijini Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Taasisi hiyo, Profesa William Pallangyo akitoa hutuba yake fupi kwenye mahafali hayo alisema kati ya watunnukiwa wa vyeti hivyo wanawake ni 3,589 sawa na asilimia 57, na wanaume 2,745 sawa na asilimia 43. Idadi ambayo inayoonesha matokeo chanya ya uwekezaji unaoendelea kufanywa katika elimu ya juu nchini.

Pallangyo alisema TIA ina kampasi katika kanda mbalimbali za Tanzania ambazo ni Dar es Salaam, Singida, Mbeya, Mtwara, Mwanza, Kigoma, Tanga na Zanzibar na kueleza kwamba ina jumla ya wanachuo 40,000. Kati yao, Kampasi za Dar es Salaam, Tanga na Zanzibar zina wanachuo 25,271, sawa na asilimia 63.2, hali inayoonesha mchango mkubwa wa kampasi hizi katika uzalishaji wa rasilimali watu wa Taifa.

Akizungumzia uboreshaji wa miundombinu ya kujifunzia na katika Kampasi za Mbeya, Mwanza na Kigoma, huku shughuli za ujenzi zikiendelea katika Kampasi za Singida, Mwanza na Zanzibar alisema jumla ya Sh. Bilioni 59 zimetumika kupitia Mradi wa HEET na mapato ya ndani ya Taasisi.

“ Sambamba na hilo, Taasisi imeimarisha matumizi ya teknolojia katika ufundishaji na ujifunzaji, ikiwemo matumizi ya Smart Boards na mifumo ya ujifunzaji kwa njia ya mtandao (e-Learning), hususan katika programu za Shahada ya Uzamili,” alisema Profesa Pallangyo.

Akizungumzia uanzishwaji wa kozi mpya alisema TIA imeanzisha kozi mpya za Shahada na Shahada ya Uzamili zinazolenga kukuza ujasiriamali, ubunifu na usimamizi wa miradi ya maendeleo, kwa lengo la kuandaa wahitimu wenye ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira na mwelekeo wa maendeleo ya Taifa. Alisema wanufaika wa mikopo ya elimu ya katika mwaka wa masomo 2025/2026, wanafunzi 14,209 wamenufaika na mikopo ya elimu ya juu, ikilinganishwa na wanafunzi 12,263 mwaka uliopita, sawa na ongezeko la asilimia 15.9 na kueleza kwamba mwaka huu wa masomo, jumla ya Sh. Bilioni 10.4 zimetolewa kugharamia masomo ya wanafunzi hao.

Aliongeza kuwa kupitia mpango huo, wanafunzi wameshiriki ziara za kielimu katika Chuo Kikuu cha Mount Kenya (Kenya) na Chuo Kikuu cha Makerere (Uganda), huku maandalizi yakiendelea ya kuwapeleka washindi wa kampasi zote jijini Pretoria, Afrika Kusini.

Aidha, Pallangyo alisema Taasisi hiyo imefanikiwa kuwawezesha wanafunzi 6 na wafanyakazi 4 kushiriki mafunzo katika Chuo Kikuu cha Vytautas Magnus nchini Lithuania, na wanafunzi wengine 2 pamoja na mfanyakazi 1 wanajiandaa kusafiri mapema mwakani.

Profesa Pallangyo aliwasihi wahitimu hao kuwa wabunifu na wabebaji wa mabadiliko chanya katika maeneo yeo ya kazi na jamii kwa ujumla.

“ Tumia elimu na teknolojia kubuni, kuboresha na kuimarisha mifumo ya kazi kwa ufanisi, uwazi na uwajibikaji. Dunia ya sasa inahitaji wataalamu wanaotumia maarifa yao kutoa suluhisho za changamoto za kijamii na kiuchumi kwa mwelekeo wa maendeleo endelevu kwani usomi na ubunifu vinaendana,”. alisema Profesa Pallangyo. Wahadhiri wakiwa kwenye mahafali hayo

Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Taasisi hiyo Profesa William Pallangyo akizungumza kwenye mahafali hayo.

Maafisa wa Jeshi la Polisi kutoka Chuo cha Taaluma cha Kurasini wakipiga saluti wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Wahadhiri wakishiriki Maandamano ya kitaaluma.

Bras Band ya Jeshi la Magareza ikiongoza maandamano hayo.
Maandamano yakifanyika.
Wahitimu wa Shahada ya Ununuzi na Ugavi wakiwa kwenye mahafali hayo.  Kushoto ni Waziri  Katanga na kulia ni Moyo Vicent
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
Ndugu, Jamaa, Wazazi, Walezi wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wasanii wa Kundi la Best Helodes Crew wa TIA Dar es Salaam wakitoa burudani
Bras Band ya Magereza ikiongoza mahafali hayo.
 

No comments