SERIKALI INAWATEGEMEA VIJANA WABUNIFU
SERIKALI inawategemea vijana wabunifu, waadilifu na watumiaji mahiri wa teknolojia
katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Hayo
yamebainishwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius
Luswetula ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 23 ya wahitimu wa
Taasisi ya Uhasibu Tanzania Kampasi za Dar es Salaam, Zanzibar na Tanga yaliyofanyika Desemba 19, 2025 Makao Makuu ya Taasisi hiyo Kurasini Jijini Dar
es Salaam.
“ Nimefurahishwa
kuona Taasisi ikiendelea kuhimiza ubunifu kupitia mashindano ya mawazo bunifu
kwa wanafunzi. Hatua hii inawajengea vijana kujiamini, kufikiri kwa ubunifu na
kuwa wazalishaji wa fursa badala ya kuwa watafuta ajira pekee,” alisema
Luswetula.
Luswetula
aliwaambia wahitimu hao kuwa katika dunia ya sasa, watumie teknolojia, hususan
Akili Bandia (AI) na mitandao ya kijamii, kubuni fursa za kiuchumi na kuongeza
kipato.
“ Vijana
wa leo wanaita hii kuwa “Content Creator” nawasihi muwe content creators wenye
tija, mnaozalisha maudhui yenye thamani, yanayoongeza kipato kwa njia halali,
kuzingatia maadili na kufuata sheria na taratibu za nchi yetu,” alisema
Luswetula na kusisitiza ‘VIJANA NI UBUNIFU, UBUNIFU NI UJANA’.
Aidha
Luswetule alitumia nafasi hiyo kutoa shukrani za dhati kwa Afisa Mtendaji Mkuu
wa TIA, Profesa William Pallangyo, Menejimenti, Bodi ya Ushauri ya Wizara,
watumishi wa Taasisi pamoja na wazazi, walezi na wadau wa elimu, kwa mchango
wao mkubwa katika kuwaunga mkono wahitimu na kuimarisha rasilimali watu kwa
Taifa.
“
Ndugu Mwenyekiti, Niwapomgeze sana kwa idadi hiyo ya wahitimu 11,382 kwenye
kampasi zote tatu. Hii inaonesha ukongwe na weledi katika utoaji wa mafunzo,
utafiti, ushauri wa kitaalam,” alisema.
Luswetula
aliongeza kuwa kwa kuzingatia muelekeo wa maendeleo na faida za kijiografia,
Dar es Salaam, Zanzibar na Tanga ni miongoni mwa maeneo muhimu yanayoendelea
kukua kwa kasi na kuwa nguzo ya uchumi wa Taifa.
Alisema
Dar es Salaam inaendelea kuwa kitovu cha biashara, bandari na huduma za
kifedha; Zanzibar ni lango muhimu la utalii, uchumi wa buluu na biashara ya
baharini na Tanga ikiwa na nafasi ya kimkakati kupitia bandari, kilimo cha
mazao ya kimkakati, viwanda na utalii wa fukwe hivyo maeneo hayo yanatoa fursa
nyingi kwa wahitimu hao kushiriki
kikamilifu katika shughuli za kiuchumi.
Afisa
Mtendaji Mkuu (CEO) wa Taasisi hiyo Profesa William Pallangyo alisema sherehe
za Mahafali hayo ya mwaka huu yamejumuisha Kampasi za Dar es Salaam, Zanzibar na Tanga ambapo
alitumia nafasi hiyo kutoa pongezi za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuchaguliwa tena kuiongoza Tanzania kwa
kipindi cha miaka mitano ijayo, pamoja na viongozi mbalimbali.
Aidha,
Pallangyo alitumia hafla hiyo kuelezea kwa kifupi baadhi ya mafanikio
yaliyopatikana na Taasisi ya Uhasibu Tanzania katika utekelezaji wa majukumu
yake ya msingi ya kutoa elimu, kufanya tafiti na kuendeleza rasilimali watu wa
Taifa.
Alisema
Taasisi hiyo ina kampasi katika kanda mbalimbali za Tanzania ambazo ni Dar es Salaam,
Singida, Mbeya, Mtwara, Mwanza, Kigoma, Tanga na Zanzibar. Taasisi ina jumla ya
wanachuo 40,000. Kati yao, Kampasi za Dar es Salaam, Tanga na Zanzibar zina
wanachuo 25,271, sawa na asilimia 63.2, hali inayoonesha mchango mkubwa wa
kampasi hizo katika uzalishaji wa rasilimali watu wa Taifa.
Maandamano ya kitaaluma yakifanyika.
Wahadhiri wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wakiwa kwenye maandamano hayo.
Muhitimu Hellen Ngete akikabidhiwa cheti pamoja na fedha.
Bras Bnd ya Jeshi la Magereza ikiwajibika katika mahafali hayo.
Wazazi, Ndugu, Jamaa na Marafiki wakiwa kwenye mahafali hayo.



Post a Comment