BALOZI DKT. NCHIMBI: CCM KUENDELEA KUMUENZI HAYATI MKAPA
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin Mkapa alipozuru katika Kijiji cha Lupaso, Masasi.
..........................
Na Mwandishi Wetu, Mtwara
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi ametembelea
kaburi la aliyekuwa Rais wa Awamu ya 3 , Hayati Benjamin William Mkapa katika
Kijiji cha Lupaso Mkoani Mtwara .Dkt Nchimbi ametembelea kaburi hilo Julai 28,
2024. na kutoa Pole kwa familia na kuzungumza na Wananchi wa Lupaso.
Balozi Nchimbi amesema "naomba nikiri kuwa Mimi ni mwanafunzi wa
hayati na nimekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa katika kipindi Chake
kwani ndio alinilipia Ada ya kusoma Chuo kikuu na alikuwa mfuatiliaji sana na
alitulea na sio Sisi lakini kwa Watanzania wote aliwalea pia alikuwa mzalendo
kwa Nchi alifanya mabadiliko Makubwa kwa Nchi yake na Kwa Chama Chake lakini
yote CCM chini ya Dkt Samia tutaendelea kuyaenzi Yale yote aliyoyoacha Hayati
Benjamin Mkapa na pamoja hayo nimeambiwa kero za hapa na tumezichukua lakini
CCM inatoa Shilingi Milioni 10 kuanza kukarabati Shule ya hapa Lupaso".
Katika ziara hii Dk Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na
Mafunzo Ndg. Amosi Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndg. Issa Ussi Haji
(Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia
Abdallah Hamid.
Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amosi Makalla akiweka shada
la maua.
Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndg. Issa Ussi Haji (Gavu) akiweka shada.
Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid akishiriki kuweka shada la maua katika
kaburi hilo.





Post a Comment