MWANAMKE AUAWA KWA KIPIGO NA MPENZI WAKE SINGIDA
Waombolezaji wakiwa mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Zainabu Mwangu (52) mkazi wa Misuna Manispaa ya Singida, anayedaiwa kufariki kutokana na kipigo cha mpenzi wake aliyekuwa akiishi naye.
KUANGALIA TUKIO ZIMA BOFYA HAPA CHINI
Na Dotto Mwaibale- SINGIDA
MWANAMKE
Mmoja mkazi wa Misuna Manispaa ya Singida, Zainabu Mwangu (52) amefariki dunia
baada ya kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake na mwanaume
aliyekuwa akiishi naye waliyemtaja kwa jina moja la Justine.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Misuna, Hamisi Lisu akizungumzia tukio hilo alisema kwamba lilifanyika usiku wa kuamkia Agosti 6, 2024 ambapo jana Julai 7, 2024 majira ya asubuhi alipigiwa simu na mjumbe wa nyumba kumi wa eneo hilo akimfahamisha kuwa katika mtaa wao kuna tukio na kabla ya kwenda eneo la tukio alimpitia mkuu wa polisi wa kata hiyo na kwenda naye ,” alisema Lisu.
Alisema
baada ya kufika nyumbani kwa marehemu akiwa ameongoza na baadhi ya ndugu zake
marehemu akiwepo mama yake walimkuta Zainabu Mwangu ( Maarufu Mama Khadija) akiwa
amelala chini sakafuni akiwa hana nguo na mwili wake ukiwa na majeraha sehemu mbalimbali
na walipomuuliza kilichomsibu aliwajibu kwa shida kwa kutamka neno moja tu simu.
Alisema walimchukua
kwenda naye Hospitali ya Sokoine akiwa hajiwezi kutokana na
maumivu makali aliyokuwa nayo na wakati akipatiwa matibabu alifariki.
Lisu alisema
asubuhi hiyo baadhi ya majirani akiwepo
baba mzazi wa marehemu walimuona mwanaume huyo aliyekuwa akiishi na marehemu akipiga
mswaki nje ya nyumba ya marehemu na walipomuuliza kuhusu hali ya mwenzake
aliwaambia kuwa hajambo.
Mjumbe wa
nyumba kumi wa eneo hilo shina namba 17, Rehema Athuman alisema walipofika ndani walikuta fimbo ambayo ilikuwa imechanika chanika ikiwa na damu
na mwili wa marehemu ukiwa una majeraha ya kama mtu aliyekuwa amekatwa katwa na
kitu kama wembe hasa sehemu za tumboni, kifuani na maeneo mengine ya mgongoni.
Baadhi ya
wanawake wa mtaa huo wameonesha kusikitishwa mno na kitendo hilo kilichopoteza
uhai wa Zaituni ambaye wamesema alikuwa akifanya kazi nyumba ya kulala wageni
ya Buziluga iliyopo mjini Singida.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Amoni Kakwale amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa taarifa kamili ataitoa baadae.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Singida, Ambwene Kajula alisema vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na jamii yote kwa ujumla havikubaliki hata kidogo na akatumia nafasi hiyo kulaani kitendo achofanyiwa Zainabu Mwangu.



Post a Comment