WATENDAJI WATAKIWA KUWA MAKINI UBORESHAJI WA DAFTARI
Na Mwandishi Wetu
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewaasa watendaji wa uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la wapiga kura kutekeleza majukumu yao kwa umakini katika
kila eneo ikiwemo utunzaji wa vifaa vya uandikishaji.
Wito huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,
Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk wakati akifungua
mafunzo ya watendaji wa uboreshaji wa Daftari ngazi ya mkoa na halmashauri za mkoa wa Dodoma leo
tarehe 14 Septemba, 2024.
“Vifaa hivi (vya uboreshaji wa Daftari) vimenunuliwa kwa gharama kubwa sana
na vinatarajiwa kutumika katika maeneo mengine ya uandikishaji nchini. Kutokuwa
makini katika utunzaji wa vifaa hivi kutapelekea athari kubwa katika
ukamilishaji wa zoezi hili muhimu.,” amesema Jaji. Mbarouk wakati akisisitiza
umuhimu wa kutunza vifaa hivyo.
Amewaasa watendaji hao kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na Tume ili
waweze kuyafanyia kazi wakati zoezi litakapokuwa limeanza.
Wakati huohuo, akifungua mafunzo kama hayo mkoani Singida, Mjumbe wa Tume
Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt. Zakia Mohamed Abubakar amesema matokeo
bora ya zoezi la uboreshaji wa Daftari yatatokana na Matokeo bora ya zoezi hili
yanategemea uwepo wa ushirikiano mkubwa kati ya watendaji wote wa uboreshaji,
serikali, vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi.
“Ninawasihi muwe na ushirikiano mzuri na wa karibu na Tume wakati wote
mtakapokuwa mnatekeleza majukumu yenu na ikiwa mnahitaji ufafanuzi au maelekezo
yeyote, msisite kuwasiliana na Tume,” amesema mjumbe huyo wa Tume.
Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya Mzunguko wa tano wa
uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao utajumuisha mkoa wa Dodoma
katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Halmashauri za Wilaya ya Bahi, Chamwino
na Kongwa, mkoa wa Manyara katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu na Wilaya ya
Kiteto na Simanjoro na mkoa wa Singida.
Uboreshaji wa daftari kwenye maeneo hayo utaanza tarehe 25 Septemba, 2024
hadi tarehe 01 Oktoba, 2024 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00
asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni. Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao ni Mratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri kutoka mkoa wa Dodoma wakila kiapo cha kujitoa uanachama na kile cha kutunza siri muda mfupi kabla ya kuanza mafunzo yao ya siku mbili kuhusu uboreshaji yaliyofanyika Makoa Makuu ya INEC jijini Dodoma Septemba 14, 2024. (Picha na INEC).



Post a Comment