MAMA LISHE DAR ES SALAAM WAKABIDHIWA MITUNGI 1000 YA GESI YA KUPIKIA KUTOKA PUMA ENERGY
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akipokea mtungi wenye gesi kutoka kwa mkaMama Lishe Mkoa wa Dar es Salaam Wapokea Mitungi 1,000 ya gesi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Fatma Abdallah (kushoto) , kushoto katika hafla iliyofanyka Oktoba 11, 2024aaaak
Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema uamuzi wa Kampuni
ya Puma Energy Tanzania kutoa mitungi 1,000 ya gesi katika mkoa huo kwa ajili
ya kuwapatia Mama Lishe kunakwenda kuchochea kasi ya safari ya kuzuia matumizi
ya nishati chafu ya kuni na mkaa.
Akizungumza leo Oktoba 11, 2024 katika viwanja Vya Biafra, Kinondoni mkoani
Dar es Salaam alipokuwa akipokea mitungi hiyo iliyotolewa na Kampuni ya Puma
Energy Tanzania, Chalamila amesema uamuzi huo umekuja wakati sahihi kwani
dhamira ya Serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imedhamiria
wananchi kutumia nishati safi ya kupikia.
Chalamila amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam ni kinara wa matumizi ya
nishati chafu, hivyo uwamuzi wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania kugawa mitungi
hiyo ya gesi itasaidia kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia na
kusisitiza kuwa kupika kwa gesi ni nafuu ukilinganisha na kuni au mkaa ambao
mbele ya safari una madhara Mengi ya kiafya ambayo yatahitaji fedha nyingi
kuyatibu.
“Dar es salaam ndio Mkoa unaotumia nishati chafu kutokana na wingi wa watu
wanaotumia kuni na mkaa kwa ajili ya kupika hivyo uamuzi huu wa Puma Energy
Tanzania unakwenda kumaliza au kupunguza matumizi ya nishati chafu katika Mkoa
wetu na Tanzania kwa ujumla.
Akigusia faida za kutumia nishati safi amesema ni pamoja na Kusaidia kuokoa
muda mwingi unaotumika kupika kwa kuni na mkaa, kuokoa gharama na kubwa zaidi
ni kuepuka madhara ya kiafya yanayosababishwa na matumizi ya kuni na mkaa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Fatma Abdallah
amesema kampuni hiyo imedhamiria kumuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan
katika kampeni ya matumizi ya nishati safi ya kupikia na ndio wameitoa mitungi
hiyo ambayo itagawanywa katika wilaya zote tanı za Mkoa huo.
“Katika Mkoa wa Dar es Salaam kuna shughuli nyingi miongoni mwa shughuli
hizo ni biashara ya chakula kinachoandaliwa kwa wingi kutoka kwa Mama Lishe
ambao wanakumbana na changamoto nyingi, mojawapo ikiwa upatikanaji wa nishati
ya kupikia, hususan nishati safi na salama,” ameeleza.
Amesema Puma Energy Tanzania inaelewa serikali chini ya Rais Samia imekuwa
na mpango kazi kwa miaka kadhaa wa kuelimisha na kueneza matumizi ya nishati
safi ya kupikia kwa wananchi wote.
Amesema Jitihada hizo zimejionyesha katika mikutano ya ndani na nje ya nchi
ambayo Rais Samia amekuwa akishiriki kuhakikisha upatikanaji na matumizi ya
nishatisafi unaimarika.
“Tunatambua wajibu wake wa kushiriki katika masuala ya maendeleo ya jamii,
hivyo itaendelea kushirikiana na serikali inayoongozwa na Rais Samia kuhakikisha
kampeni ya nishati safi inafanikiwa kwani dhamira ya Rais ifikapo mwaka 2034
asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi na sisi tuko naye kufikia
malengo hayo,” amesema.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akikabidhi mitungi hiyo.
Picha ya pamoja wakati wa makabidhiano ya mitungi hiyo yenye gesi
Hafla ya makabidhiano ikiendelea.
Wanawake wakionesha furaha zao wakati wa zoezi la kugawa mitungi hiyo
Picha ya pamoja









Post a Comment