Header Ads

PROMOSHENI YA BIA YA WINDHOEK KUTIKISA TEXAS BAR NA NIGHT CLUB GOBA JIJINI DAR ES SALAAM




Muuonekano wa Bia aina ya Windhoek

................................... 

Na Dotto Mwaibale.

LEO katika kiota cha maraha Texas Bar na Night Club iliyopo Goba jijini Dar es Salaam kuanzia saa 8 mchana huu kutakuwa na Prosheni kubwa ya aina yake ya vinywaji mbalimbali vya kisasa vinavyosambazwa hapa nchini na Kampuni ya Heineken Beverages ambayo ni maarufu duniani kwa uuzaji wa vinywaji.

Moja ya kinywaji kitakachokuwepo kwenye promosheni hiyo ni Bia aina ya Windhoek ambayo ni ya hali ya juu inayotengenezwa nchini Namibia ikiwa na ladha nyororo, ya kuburudisha, inayoheshimika kuwa ni bia bora zaidi, na iliyo na ubora kamili inayopatikana kila kona ya Tanzania kwa bei nafuu na kupendwa na idadi kubwa ya watanzania.

Moja ya sifa kubwa ya bia hiyo ni kutokuwa na ‘eng’iova’ kwa mnywaji ambae akiamka asubuhi anajisikia vizuri na kumfanya aendelee na shughuli zake akiwa na furaha.

Afisa mmoja wa kampuni hiyo ya Heineken Beverages ambaye hakupenda jina lake liandikwe akizungumzia promosheni hiyo alisema itaanza saa nane mchana wa leo Mei 24, 2025 na itaendelea hadi saa sita usiku na kuwa kesho itafanyika tena katika eneo hilo la Goba na kueleza kuwa itakuwa endelevu.

Alisema promosheni hizo zimelenga kutangaza vinywaji hivyo pendwa ambavyo vikinunuliwa kwa wingi vitachangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

Aidha ametoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam na vitongoji vyake hasa vya Goba kufika Texas Bar na Night Club kushiriki promosheni hiyo.

Kwa upande wake Meneja wa Bar hiyo Tito Justine amesema wadau mbalimbali watakaofika kwenye promosheni hiyo wafike kwa wingi kufurahi huduma zilizopo kama ya vyakula vya aina mbalimbali vilivyoandaliwa na wapishi wa viwango vya juu.

Alitaja huduma zingine ambazo zipo kwenye bar hiyo kuwa ni ya Cassino, Car Wash, Live Band inayoporomoshwa na Bendi ya Mwenge Jazz kila Jumamosi huku kukiwa na nafasi kubwa ya kuegesha magari na kuwa na ulinzi wa kutosha.

Alisema katika bar hiyo kuna hali nzuri ya usalama hivyo aliwaomba wadau hao kufika kwa wingi kushiriki promosheni hiyo.

Muonekano wa Kiota cha maraha Texas Bar and Night Club iliyopo Goba jijini Dar es Salaa.

No comments