PROMOSHENI ZA WINDHOEK, TEXAS BAR AND NIGHT CLUB GOBA JIJINI DAR ES SALAAM ZANOGESHA BAR HIYO
Na
Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
PROMOSHENI
ya bia ya Windhoek inayoendelea kufanyika eneo la maraha yaani Texas Bar na
Night Club iliyopo Goba jijini Dar es Salaam zimeinogesha bar hiyo na kuwa
kimbilio la watu wengi kwenda kupumzika na kujipatia vinywaji vya kisasa vinavyosambazwa
nchini na Kampuni ya Heineken Beverages ambayo ni maarufu si kwa Tanzania pekee bali duniani
kote kwa uuzaji wa vinywaji.
Leo
tena katika bar hiyo ya maraha kuanzia saa 8 mchana huu kutakuwa na Promosheni
kubwa ya aina yake ya vinywaji mbalimbali vya kisasa ikiwemo bia ya Windhoek
ambayo imekuwa ikichangamkiwa na wanywaji kutokana na ubora wake wa kimataifa.
Bia hiyo ya
Windhoek Lager ambayo ina ubora wa hali ya juu inatengenezwa nchini Namibia na
kutokana na ubora wake imeenea duniani kote.
Kinywaji
hicho kina ladha nyororo, ya kuburudisha, inayoheshimika kwa ubora zaidi
ambacho hapa nchini kinapatikana kila kona kwa bei nafuu na kupendwa na idadi
kubwa ya watanzania.
Moja
ya sifa kubwa ya bia hiyo ambayo imejizolea umaarufu ni kutokuwa na ‘eng’iova’
kwa mnywaji ambae akiamka asubuhi baada ya kuinywa anajisikia vizuri na
kumfanya aendelee na shughuli zake akiwa na furaha.
Afisa
mauzo wa kampuni hiyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe alisema promosheni
hizo zimelenga kutangaza vinywaji hivyo pendwa ambavyo vikinunuliwa kwa wingi
vitachangia ukuaji wa uchumi wa nchi.
“ Bei
ya bia hii ya Windhoek katika promosheni yetu ni ya chini kabisa kwani katoni
moja yenye bia sita ambayo kwa kawaida inauzwa Sh. 24,000 kwa bei ya promosheni
tunauza Sh.20,000 yaani ni bei rafiki kabisa kwa wanywaji,” alisema Afisa huyo.
Aidha ametoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam na vitongoji vyake hasa vya Goba kufika Texas Bar na Night Club kushiriki promosheni hiyo.
Meneja wa Bar hiyo
Tito Justine amesema promosheni zinazoendelea za bia hiyo zimechochea ongezeko
la wadau wanaofika kwenye bar hiyo kwa wingi na kufurahiya huduma zilizopo kama
ya vyakula vya aina mbalimbali na nyama choma za aina zote vinavyoandaliwa na
wapishi wenye uzoefu wa viwango vya hoteli ya nyota tano.
Alitaja huduma zingine ambazo zipo
kwenye bar hiyo kuwa ni ya Cassino, Car Wash, Live Band inayoporomoshwa na
Bendi ya Mwenge Jazz kila Jumamosi huku kukiwa na nafasi kubwa ya kuegesha
magari na kuwa na ulinzi wa kutosha.
Alisema kwa walaji wa mbuzi katoliki
‘Kitimoto’ pia kinapatikana katika eneo maalumu lilitengwe katika bar hiyo na
kufanya kila mtu kufurahia weekend yake akiwa katika bar hiyo yenye mandhari na
rafiki kwa mapumziko.
Baadhi ya wateja wameupongeza uongozi wa bar hiyo kwa ushikiano mkubwa na kampuni hiyo na kufanya promosheni ya vinywaji vyao wakati wowote na wafurahiye mapumziko yao ya mwishoni mwa wiki.
Muonekana wa Texas Bar and Night Club iliyopo Goba jirani na mzunguko wa magari barabara ya kutoka Makongo na ile ya kwenda Mbezi.Hiki ndio Texas Bar and Night Club kiota cha maraha kilichopo Goba.





Post a Comment