SERIKALI YATOA VYOMBO VYA USAFIRI TANESCO MKOA WA SINGIDA
SERIKALI ya Jumhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa vyombo vya usafiri kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mkoa wa Singida kwa ajili ya kuboresha utendaji wa kazi.
Mkuu wa Mkoa
wa Singida, Halima Dendego akizungumza wakati akikabidhi vyombo hivyo amepongeza
kazi kubwa inayofanywa na shirika hilo chini ya Mkurugenzi Mtendaji wake Lazaro
Twange kwa maboresho makubwa anayofanya
Mhe. Dendegu
ametoa pongezi hizo Aprili 30, 2026 wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vyombo hivyo
vya usafiri (Magari Manne) ambayo
yanakwenda kutoa huduma kwa wananchi.
“Awali ya yote nichukue nafasi hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali anayoingoza kwa jitihada kubwa anayoifanya ya kuwajengea uwezo watumishi, kuwapeleka shule. kuongeza wafanyakazi wapya na kuwaletea vitendea kazi, huu ni uwekezaji mkubwa unaofanywa ili muweze kufanya kazi vizuri,” alisema Dendego.
Aidha,
alipongeza Tanesco Singida kwa kazi kubwa wanayoifanya chini ya Meneja wa
shirika hilo mkoani humo, Mhandisi Mwamvita Ally na timu yake na kueleza kuwa
tangia afike Singida hajawahi kuona changamoto kubwa ya umeme isipokuwa ile ya jumla.
Alisema
changamoto siku zote zipo, akitolea mfano mvua zinaponyesha nguzo zinaanguka na
nyingine nyingi lakini anafurahi anapoona zinapotokea wanapata taarifa na hatua
za kuzitatua zinapofanyika kwa wakati.
“Ikitokea hitilafu tu mnatuambia na mnaifanyia kazi kwa wakati haya ni mapinduzi na mageuzi makubwa ya kiutendaji ndani ya Tanesco,” alisema Dendego.
Aliongeza
kuwa hivi sasa umeme siyo anasa ni uchumi na ndiyo kila kitu, hivyo
tunapotekeleza dira ya Taifa ya 20 / 50 malengo yetu yatafikiwa kwa nyinyi
kuhakikisha tunapata huduma ya umeme wa kutosha ambapo pia alihimiza magari
hayo yatunzwe.
Kwa upande
wake Meneja wa shirika hilo Mkoa wa Singida, Mhandisi Mwamvita Ally aliishukuru
Serikali chini ya Rais Samia kwa kuwapatia magari hayo ambapo aliahidi
kuyatunza na kuhakikisha yatatumika kwa ajili ya kuwahudumia wananchi.
Afisa
Usalama wa shirika hilo Mkoa wa Singida, Emilini Ndahani aliishukuru Serikali
kwa kuwapa magari hayo na kueleza kuwa watahakikisha yanatumika kwa kazi
iliyokusudiwa.
“Tunamshukuru sana mkurugenzi wetu Lazaro Twange kwa jitihada alizofanya na kutupatia magari haya ambayo yanakwenda kutoa huduma kwa wananchi na tutazingatia usalama wake pamoja na watu kwa kuwaelekeza madereva matumizi bora ya magari hayo,” alisema Ndahani.
Naye
Mhandisi Boniface Shitindi wa shirika hilo Mkoa wa Singida alimshukuru Rais
Samia kwa kuwashika mkono na kuweza kutoa magari hayo ambayo yanakwenda kuwapa
tija ya kikazi.
“ Jambo ili kwetu ni chachu ya kuongeza uchumi wa Taifa letu kama kauli mbiu yetu inavyo sema “Tunayaangaza Maisha” ndivyo tunavyoendelea kuyaangaza kupitia magari hayo tuliyopatiwa na Serikali.
Vyombo vya usafiri vilivyo kabidhiwa ni Land Cruiser mbili mpya na mashine mbili za kuinua vitu vizito zikiwemo nguzo.
Taarifa hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale namba ya simu 0754362990.










Post a Comment