Header Ads

SIMULIZI YA MWANAHARAKATI PATRICK GEORGE MITRI

Awasaka viongozi wa Kitaifa kwa miaka 13 awape waraka bila mafanikio


 Patrick George Mitri

.........................

Misukumo ya kitaifa ilinizidi kila wakati nilipokata tamaa na kuona kilichondani yangu ni kigumu kwangu na ndipo nilipoomba ushauri kwa watu wa karibu yangu wenye upeo ulionizidi, ushauri wao uliangukia neon moja nianzishe Shirika lisilo la Kiserikali (NG’Os) ndiyo nitaweza kuionesha jamii kipaji changu na kuwatumikia.

Sikuchelewa niliingia kwenye wajibu wa kutafuta watu niwape wazo langu ambapo ulitokea ugumu na msukumo ulinielekeza nipate watu ambao hawajawai kujiunga na vyama vya siasa toka wazaliwe kama mimi, wawe ndio waanzilishi wa shirika hilo (ASASI).

Nilifanikiwa kuwapata licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa ambapo niliwashauri na kunielewa.

Baada ya hapo tulikuwa na majukumu matatu ambayo ni kama ifuatavyo:

1.Kuunda kikundi cha Vita dhidi ya umasikini.

2.Kutengeneza katiba

3.Kusajili shirika la vita dhidi ya umasikini kitaifa.

 

Tulifanikiwa kwa kiwango kikubwa ikapatikana katiba ambayo ilipitishwa kwa mujibu wa sharia na kuipeka Wizara ya Mambo ya Ndani Jijini Dar es Salaam.

Kwa bahati mbaya nilipofika mapokezi na kupokelewa katiba ili nipate maelezo wafanyakazi wa kitengo cha mapokezi walipata taarifa ya msiba wa mfanyakazi mwenzao ambaye alikuwa ni mwanamke tukio hilo kwao lilikuwa la ghafla kwani niliona hadi wanaume wakitoka machozi ambapo sikupata maelezo yoyote zaidi ya kukabidhi katiba na kuacha namba yangu ya simu kwa taarifa zaidi.

Baada ya hapo nilitafuta usafiri na kurudi nyumbani Korogwe nikiwa nimechoka na kukata tamaa.

 

NAMBA 3

Niliporudi nyumbani ninakoishi Kijiji cha Mgila Korogwe Vijijini, usiku nilipata msukumo ulionionesha ninafanya kosa kubwa kitaifa kwa wakati ule kufuatilia usajili wa Shirika.

Niliona nguzo tatu ambazo ni Muhimiri wa Taifa na zile nguzo niliziona zilivyo ambazo ni kama ifuatavyo:

1.Dini

2.Siasa

3. Ulinzi na Usalama.

Usiku ule kunakitu nilichokibaini ambacho ni jambo kubwa la kitaifa kama hili la vita dhidi ya umasikini lina shabaha kubwa ni lazima lipite kwa makundi hayo matatu na kueleweka kwao mwanzo na mwisho wake walichakate, walichuje na hatimaye wawe na jibu moja kama linafaa kitaifa ndipo lifuate utaratibu wa kisheria wa kuanzishwa Shirika hilo la kitaifa na kama halifai lisuruhusiwe kuanzishwa kwa maslahi ya taifa.

Kwa sababu waliondani ya usimamizi wa mihiri hiyo mitatu ya taifa ndiyo wanaobeba lawama taifa likiyumba na pia ubeba heshima na sifa njema taifa liking’aa.

Niliona wajibu wao wa haki kuchuja kwa pamoja masuala makuu ya kitaifa kabla hayajafika ngazi ya mujibu wa sheria kwa kuanzishwa mashirika ya kiraia ndiyo ikawa mwisho wa wazo la kuanzisha shirika hilo nisijue la kufanya huku msongo wa mawazo ukitamalaki na kukata tamaa.

Simulizi ya pili, itaendelea tena kesho kwa maoni piga namba 0717356133.  

No comments