MWENYEKITI WA WATU WENYE ULEMAVU MKOA WA DAR ES SALAAM KUFUNGA NDOA
......................................
MWENYEKITI wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Dar es Salaam (SHIVYAWATA), Charles Matemba anatarajia kufunga ndoa na Fatuma Ally Makame Juni 27, 2026, Halmashauri ya Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
Wanandoa hawa watarajiwa ni watu wenye ulemavu, wameamua kuwa pamoja katika maisha yao ya ndoa jambo ambalo ni jema.
"Tumeamua kufunga ndoa sisi wenye ulemavu kwani watu wenye ulemavu wana moyo wa kupenda na wana hisia kama wawalivyo wengine, "alisema Matemba.
Bwana harusi huyo mtarajiwa akizungumza na waandishi wa habari Mei 17, 2026 katika kikao cha kamati ya maandalizi ya harusi yao kilichofanyika Magomeni jijini Dar es Salaam alisema ameguswa kumuoa mlemavu mwenzake kwani wenye ulemavu wamekuwa katika mazingira ya kunyanyapaliwa kutokana na hali yao kwamba hawawezi kuoa au kuolewa.
Aidha, Matemba ametumia nafasi hiyo kuwaomba ndugu, jamaa, marafiki na wadau mbalimbali kuwashika mkono (kuwachangia), kwa hali na mali ili kufanikisha tukio hilo ambalo muda wake umebaki mchache.
Kwa upande wake Bibi harusi mtarajiwa Fatuma Makame amesema ameamua kuolewa na Charles Matemba ambaye ni mtu mwenye ulemavu kama yeye kwa kuwa ni mwanadamu mwenye hisia kama walivyo wengine.
"Nimeamua kuoana na Bwana Matemba kwani ninaamini tutasaidiana katika shida na raha," alisema Makame.
Watarajiwa hao wametoa wito kwa jamii kuwa watu wenye ulemavu wanaweza kufanya mambo mbalimbali kama ilivyo kwa watu wengine hivyo wasikate tamaa bali wasonge mbele.
Naye Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya harusi hiyo, Vaileth Mwazembe amesema anaiomba jamii kuwachangia maharusi hao watarajiwa kwa chochote ili waweze kufanikisha jambo hilo.
"Nawaomba jamii kuwa bega kwa bega na maharusi hawa watarajiwa kwa kuchangia chochote kile ili kufanikisha jambo hili la baraka, " alisema Mwazembe.
Ili kufanikisha shughuli hiyo tunaomba mchango wako kwa kuwa mahitaji ni mengi na bado hakuna kitu chochote kilichofanyika kwani ndiyo kwanza wapo kwenye vikao vya awali.
Kwa yeyote ambaye ataguswa na atakuwa tayari kuwachangia atume mchango wake kwa namba ya Tigo Pesa-0676701819 na MPESA -0766101802 Jina Charles Matemba.
Bwana harusi Mtarajiwa Charles Matemba akiwa katika ubora wake.





Post a Comment