Header Ads

REGINA NDEGE MBUNGE MWENYE UPENDO ANAYEGUSA MAISHA YA WATU MANYARA


Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Manyara na Naibu  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe. Regina Ndege, akimjulia hali Mama Mzazi wa Mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Manyara, Inyasi Mpaki na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Wilaya ya Babati Vijijini, Solomon Mpaki ambaye amelazwa Hospitaaali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma anasumbuliwa na nyonga.

...........................

UPENDO ni hali ya moyo wa mtu kuwa na hisia kali ya  kujali, kuhurumia kuwa na uchungu dhidi ya mtu mwingine bila ya kinyongo.

Ni sifa ya thamani inayohusisha ustahimilivu  na kutafuta mema kwa wengine kama biblia inayoeleza upendo kama amri kuu, ikimaanisha ni msingi wa maisha ya kiroho.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Manyara na Naibu  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe. Regina Ndege ni kiongozi mwenye upendo ambaye anagusa maisha ya watu.

Wananchi wa Mkoa wa Manyara wanamuita Mama wa Faraja wa mkoa ho.

Mhe. Ndege wakati wote amekuwa mstari wa mbele kushirikiana na wananchi katika mambo mbalimbali ya maendeleo, furaha na huzuni.

Jambo hilo limekuwa likimuweka jirani zaidi na wananchi na kufanya apendwe.

Mhe. Ndege kutokana na hulka yake ya kuwa na wananchi karibu amekuwa akiweka kipaumbele hasa wanapokuwa na changamoto mbalimbali zikiwepo za ugonjwa.

Kiongozi huyu amekuwa hapoi katika shughuli mbalimbali zinazowahusu wananchi ambapo leo  alikwenda Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma  kumjulia hali Mama Mzazi wa Mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Manyara, Inyasi Mpaki na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Wilaya ya Babati Vijijini, Solomon Mpaki ambaye anasumbuliwa na nyonga.

 “Maisha ya Mhe. Ndege yamekuwa kielelezo kwa wana Manyara na Taifa kwa ujumla hasa katika masuala ya siasa na kijamii,” alisema Kulwa Mkamba.

Mkamba alisema mambo  anayofanya Mhe. Ndege yamekuwa ni darasa kwa watu mbalimbali siyo tu wa Mkoa wa Manyara bali Tanzania kwa ujumla.

Mhe. Regina Ndege, akimjulia hali Mama huyo. Wengine ni Wajumbe wa Baraza la Wazazi kutoka Mkoa wa Manyara. 
Mhe. Regina Ndege, akimjulia hali Mama huyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Wilaya ya Babati Vijijini, Solomon Mpaki.

.....................................

Taarifa hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale simu namba 0754362990.
 

No comments