TIA YAJIVUNIA HATUA UBORESHAJI MIUNDOMBINU KATIKA KAMPASI ZAKE
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Profesa William Pallangyo akizungumza wakati akitoa taarifa kwenye mahafali ya kihistoria baada ya Kampasi ya Singida kutoa kundi la kwanza la Wahitimu wa Shahada ya Uzamili yaliyofanyika Juni 5, 2026 mkoani Singida.
............................
Na Mwandishi Wetu, Singida
TAASISI ya
Uhasibu Tanzania (TIA) yajivunia uboreshaji wa miundombinu ya kufundishia na
kujifunzia katika kampasi zake.
Hayo
yamebainishwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa William Pallangyo wakati
akitoa taarifa kwenye mahafali ya kihistoria baada ya Kampasi ya Singida kutoa kundi la kwanza la Wahitimu wa Shahada ya Uzamili.
Wahitimu 548
kutoka Kampasi za Dar es Salaam, Zanzibar, Mtwara, Kigoma na Singida
walitunukiwa Shahada za Uzamili katika Mahafali ya 24 yaliyofanyika Juni 5,2026
Manispaa ya Singida.
Akizungumza kwenye mahafali hayo Profesa Pallangyo alisema Taasisi hiyo imeendelea kupiga hatua kubwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya msingi sambamba na uboreshaji wa miundombinu ya kufundishia na kujifunzia.
“Mafanikio
haya yanatekelezwa kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu kupitia Mradi wa Mageuzi ya Kiuchumi kwa Vyuo vya Elimu ya Juu (HEET) unaosimamiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,” alisema.
Pallangyo
alitaja miongoni mwa mafanikio hayo yaliyopatikana kuwa ni Ujenzi wa Jengo la
Taaluma katika Kampasi ya Singida (shilingi bilioni 13.5) ambao umefikia
asilimia 60.
Alitaja maendeleo
ya kampasi nyingine kuwa ni ya Mwanza ambako kuna ujenzi wa hosteli mbili za
wanafunzi ambazo zimegharimu Shilingi bilioni 7.2 na ujenzi wake umefikia asilimia 95
ya utekelezaji.
Alisema, Pia Taasisi hiyo ina miradi
mingine inayotekelezwa ambayo ni ujenzi wa majengo ya taaluma na utawala katika Kampasi ya Kigoma kwa gharama ya Shilingi
bilioni 11.08 ambayo yamekamilika kwa asilimia 98.
Ujenzi wa majengo ya taaluma, utawala na mabweni katika Kampasi ya Zanzibar kwa gharama ya Shilingi bilioni 15.9 ujenzi wake unaendelea na umefikia asilimia 30 ya utekelezaji.
Kukamilika kwa
miundombinu hiyo, kunaiwezesha Taasisi kuongeza udahili sambamba na ubora wa
huduma za mafunzo.
Alisema kwa mwaka 2025/2026 Taasisi imefanya zaidi ya tafiti 13 na kuzalisha machapisho 60 ya kitaaluma katika maeneo mbalimbali.
Alisema Watumishi
24 wanaendelea na masomo ya Shahada ya Uzamivu (PhD) katika vyuo mbalimbali
nchini na nje ya nchi.
Mkuu wa Mkoa
wa Singida, Halima Dendego ambaye alikuwa mgeni rasmi akifungua program ya
mafunzo ya uzamili katika mahafali hayo alisema ni hatua muhimu kwa mkoa wa
Singida katika kuendelea kuzalisha wataalamu bobezi wanaohitajika katika sekta
mbalimbali za umma na sekta binafsi.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa TIA Kampasi ya Singida
Picha ya pamoja na wahitimu
Maandamano yakifanyika kueekea eneo lililoandaliwa kwa ajili ya mahafali hayo
Maandamano yaakiendelea
Bras Bend ikiongoza maandamano hayo
Wahadhiri wakiwa na mgeni rasmi kabla ya kupokea maandamano ya wahitimu
Wahadhiri wakiwa tayari kupokea maandamano ya wahitimu
Wahitimu wakitunukiwa Shahada ya Uzamili.
Wahitimu wakitunukiwa Shahada ya Uzamili.
Mahafali yakiendelea
Bras Bend ya Magereza ikitoa burudani kwenye mahafali hayo

















Post a Comment