WAZIRI NDUMBARO AZUHIA UJENZI WA SHULE ENEO LA MICHEZO
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na wanananchi na kuagizwa kusitishwa kwa ujenzi wa shule ya msingi katika eneo la michezo lililopo mtaa wa Panga, Tegeta Wazo jijjini Dar es Salaam leo Agosti 12, 2024.
...................................
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro ameagiza kusitishwa mara moja kwa ujenzi wa shule ya msingi katika eneo la michezo lililopo mtaa wa Panga, Tegeta Wazo Jijjini Dar es Salaam.
Ndumbaro amefikia uamuzi huo kufuatia pingamizi la wananchi wa eneo hilo kukataa ujenzi wa shule hiyo katika eneo hilo ambalo limekua likitumika kwa shughuli za michezo tangu awali.
Hata hivyo, Waziri Ndumbaro amewataka viongozi wa kata hiyo na wananchi kutafuta eneo lingine ambalo litatumika katika ujenzi wa shule hiyo ambapo pia ametoa siku tatu kwa mkandarasi na viongozi wa Halmashauri kurudisha uwanja katika hali yake ya kawaida ili uendelee kutumika kwa michezo.








Post a Comment