CCM KIGOMA YAFANYA UTEUZI WAGOMBEA NAFASI YA UDIWANI, UCHAGUZI KUFANYIKA JUNI MOSI , 2026
....................................
Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa kigoma
imefanya uteuzi wa wagombea wa nafasi za udiwani katika uchaguzi mdogo wa
udiwani katika kata za Nyamgali wilayani Buhigwe na Nyumbigwa wilayani Kasulu.
Katibu wa siasa, uenezi na mafunzo wa CCM Mkoa wa kigoma
Deogratius Nsokolo amesema, Katika kikao hicho ambacho kimeongozwa na
mwenyekiti wa CCM Mkoa Jamal Tamim kimemteua Ludovick Nyaruguru Boyi kugombea
katila kata ya Nyumbigwa wilayani Kasulu na Anania Jest Mbango kuwania udiwani katika kata ya Nyamgali
wilayani Buhigwe.
Uchaguzi katika kata hizo utafanyika Juni Mosi mwaka huu na
unafanyika kufuatia vifo vya madiwani wa kata hizo .
Halmashauri kuu ya CCM Mkoa pia imeweka mikakati kadhaa ya kuimarisha Chama.
Viongozi wa CCM Mkoa wa Kigoma wakiwa kwenye kikao hicho cha uteuzi. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma Comred Jamal Tamim, kushoto kwake ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa Abdulkadri Mushi na kulia kwake ni Katibu wa CCM waMkoa huo, Christopher Palangyo.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoaa wa Kigoma wakiwa kwenye kikao hicho.





Post a Comment