ULEGA, DIWANI KATA YA VIKINDU VIONGOZI WA MFANO, WASIKIVU KWA WANANCHI
Kiongozi
huyu huongoza kwa vitendo badala ya maelekezo tu, akijenga mazingira ya
kuaminiana na kutoa mwelekeo chanya.
Mbunge wa
Jimbo la Mkuranga ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, Mhe.Abdallah Hamisi Ulega na
Diwani wa Kata ya Vikindu, Mohamed Maundu ni viongozi wa mfano, wanaojali na ni
watu wenye upendo, huruma, na wanaothamini uwepo wa watu wengine bila kujali
maslahi binafsi.
Mhe. Ulega
licha ya kuwa na majukumu mengi ya kitaifa kupitia nafasi yake ya Uwaziri
amekuwa mtu wa kujali changamoto mbalimbali za wananchi wake jimboni.
Kwa muda
mrefu hasa kipindi cha mvua za masika wakazi wa Kitongoji cha Mpera kilichopo Kijiji cha
Kisemvule Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani walikuwa katika changamoto kubwa
kutokana na kutokuwa na barabara ya
uhakika baada ya karavati linalounganisha maeneo hayo kusombwa na maji.
Wananchi hao
wameanza kupata matumaini makubwa baada ya mbunge wao kusikikia kiliochao na
kuanza kujenga karavati hilo hatua ambayo imewafurahisha.
Hali ya
kutokuwepo kwa karavati hilo iliwafanya wananchi hao kutumia gharama kubwa ya
usafiri kufuatia eneo hilo kutegemea usafiri wa bodaboda pekee.
Mkazi wa
eneo hilo ambaye hakupenda kutaja jina lake akizungumza na Mwandishi wetu, Mei
14, 2026, alisema kukosekana kwa barabara hiyo kumechangiwa na mvua
zinazoendelea kunyesha kusomba karavati
la mto Bavu linalounganisha Kijiji cha Kisemvule na kitongoji hicho.
Hussein Jongo ambaye ni mkazi wa kitongoji
hicho, alisema licha ya changamoto ya barabara katika shule za eneo hilo
kunaukosefu mkubwa wa miundombinu ya madarasa na madawati kwani wanafunzi wanakaa chini.
Kwa upande
wake Juma Koleza alisema changamoto ya barabara katika eneo hilo ni kubwa
ingawa jitihada ndogo ndogo zimekuwa zikifanyika hasa kwenye karavati la mto
Bavu.
Alisema eneo
hilo limekuwa likijengwa mara kwa mara na mara ya mwisho Mwenyekiti wa Kijiji hicho
alifanya jitihada za kukata magogo ya minazi ili yasaidie watu kupita lakini
nayo ilisombwa na maji na sasa linatumika daraja la muda la miti ambalo magari
hayawezi kupita zaidi ya bodaboda au Toyo.
“Changamoto
hii inafahamika hadi Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga kinachosubiriwa mvua
ziache kunyesha ndipo waanze ujenzi wa daraja,” alisema Koleza.
Diwani wa
Kata ya Vikindu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mohamedi Maundu akizungumzia
kuhusu changamoto hiyo alisema mipango waliyonayo na Mbunge wa Jimbo la Ulega
ambaye ni Waziri wa Ujenzi ni kwenda kujenga karavati katika eneo hilo hatua.
“Mpango wetu
ni kwenda kujenga karavati katika eneo hilo na tayari tumekwishapata karavati
la dharura na ndani ya siku tatu ujenzi wa karavati hilo utakuwa umekamilika,”
alisema Maundu.
Ni hatua
nzuri iliyofanywa na Mhe. Ulega pamoja na Diwani wa Kata ya Vikindu kwani Mei
16, 2026 siku mbili baada ya mwandishi wetu kuzungumza na wananchi kuhusu kero
hiyo walipeleka karavati na kuanza ujenzi mara moja na kudhibitisha kwa vitendo
kuwa ni viongozi wa mfano na wasikivu katika kuwatumikia wananchi.
“Mbunge wetu
Abdallah Ulega na diwani Maundu hakika wanakwenda na kasi ya utendaji kazi ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan,” alisema Hawa
Omari mkazi wa kata hiyo.
...................................
Taarifa hii imeandikwa na Dotto Mwaibale namba ya simu 0754362990.





Post a Comment